STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 15 Mei 2016

REKODI MBALIMBALI KATIKA LIGI KUBWA NNE BARANI ULAYA SIKU YA JANA...............

 




Siku ya Jumamosi ya tarehe 14/5/2016 tumeshuhudia ligi mbalimbali zikiendelea katika michezo ya mwisho msimu wa 2015-2016.

Stori kubwa ni rekodi mbalimbali zilizowekwa kule Nchini Ufaransa,Hipania,Italia na Ujerumani katika ligi kuu za mataifa hayo.

                            UFARANSA-LIGUE 1  



Ibrahimovic celebrates winning the Ligue 1 title with Paris Saint-Germain as the likes of David Luiz and Angel Di Maria join the party


 Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic akiinua taji la Ligue 1 na wachezaji wenzake wa Paris Saint-Germain Uwanja wa Parc des Princes baada ya kuisaidia timu yake hiyo kutwaa tena ubingwa wa Ufaransa, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nantes, yeye akifunga mabao mawili. Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Lucas Moura na Marquinhos

Ibrahimovic set a record for league goals in a single season by a Paris Saint-Germain player with his two strikes against NantesMabao ya Ibrahimovic yakamwezesha kumaliza msimu kwa kufunga magoli 38 na kuvunja rekodi ya  Carlos Bianchi ambapo alimaliza msimu kwa kufunga magoli 37 msimu wa  1977-78  



                                                   ITALIA- SERIA "A




Higuain,28 ameibuka kinara wa upachikaji mabao baada ya kufunga magoli 36 katika michezo 35 ya Seria A baada ya jana Jumamosi kufunga mabao matatu (hat-trick) na kuiongoza Napoli kuchomoza na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Frosinone. 



Higuain makes Serie A history by breaking 66-year-old goalscoring record

Magoli hayo yamemfanya Higuain aweke rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi katika ligi hiyo ndani ya msimu mmoja akiivunjwa rekodi iliyodumu kwa miaka 66 ya Gunnar Nordahl ya msimu wa 1949-50 ya mabao 35 aliyoiweka akiwa na AC Milan.


                            UJERUMANI-BUNDESLIGA
 The outgoing head coach celebrates his side's success with Bayern Munich player Holger Badstuber after the game on Saturday 
Ligi kuu ya Ujerumani mabingwa ni Bayern Munich wakifanikiwa kutetea ubingwa wao,lakini tukio kubwa lilijitokeza kwenye mchezo wa Bayern Munich walipokuwa wanacheza na Hannover 96 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

It was not only the manager who was presented with a trophy as Lewandowski collected his top scorer award before kick-off
Wafungaji walikuwa ni R.Lewandowski aliefunga dakika ya 12 kisha Gotze dakika ya 28 na 54 goli pekee la Hannover likafungwa na Sobiech dakika ya 66.

Goli la Robert Lewandowski lilimfanya kufikisha magoli 30 katika ligi na kuwa mfungaji bora wakati huo pia akiwa ni mchezaji pekee kufikisha magoli 30 kwenye msimu mmoja wa Bundesliga baada ya miaka 39 mara ya mwisho kwa mchezaji kufunga magoli 30 na zaidi ni Dieter Müller (34) wa Fc Koln msimu wa 1976-77.
 
                                                         HISPANIA-LA-LIGA;

Mshambuliaji wa Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia timu yake mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika mchezo wa La Liga usiku wa Jumamosi. 
Kwa mabao hayo, Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kihistoria kufunga mabao zaidi ya 50 kwa misimu sita mfululizo.

Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez akiruka hewani kushangilia baada ya kuifungia timu yake mabao yote matatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Granada kwenye mchezo wa La Liga usiku wa Jumamosi Uwanja wa Nuevo Los Carmenes. 
 
 


Ushindi huo umeifanya Barca kufikisha pointi 91 baada ya kucheza mechi 38 na kutwaa ubingwa wa La Liga, wakiwazidi kwa pinti moja mahasimu, Real Madird.







Wakati huo pia Dani Alves ameipiku rekodi ya gwiji  Pele ya kuwa mchezaji kutokea nchini Brazil aliechukua mataji mengi zaidi
Mpaka sasa amechukua mataji 30huku  Pele, akifanikiwa kuchukua mataji 29 .

Dani Alves overtakes Pele as the most successful Brazilian 
Alves pia alifikisha assistya  100 katika  La Ligakwenye goli la pili la Suarez na kushika nafasi ya tatu nyuma ya  Lionel Messi na  Luis Figo.


 Golikipa wa Atletico Madrid J.Oblack ndie ambae ana clean sheet nyingi katika msimu huu kwenye ligi kubwa tano Barani Ulaya akiwa nazo 24 akifuatiwa na G.Buffon (21),M.Neur (20) na K.Trapp (18).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox