MWISHONI mwa wiki iliyopita, aliyekuwa beki wa Simba, Hassan Kessy alimwaga wino wa kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.
Kessy ameondoka Simba wakati ambao mashabiki wa timu
hiyo bado wanamuhitaji tena zaidi ya sana.
Mashabiki wa Simba walikuwa bado wanamuhitaji Kessy kwa
sababu timu yao haipo vizuri katika ushindani halafu ghafla mchezaji muhimu
kama yeye anaondoka, lazima iwe anguko.
Haukuwa muda sahihi kwa Kessy kuondoka Simba, lakini
jeuri ya viongozi wa klabu hiyo ndiyo umesababisha hayo yote.
Mchezaji mwenyewe alikua bado anaipenda timu yake hiyo, lakini kwa mambo aliyokua akifanyiwa akaona isiwe shida, akawaachia timu yao.
Kessy ameondoka, nani anafuata? Hilo swali lipo vichwani
mwa watu wengi ambao ni wanafamilia wa soka hapa nchini.
Kuna tetesi kwamba straika wao, Ibrahim Ajib naye anatakiwa na Yanga, tusubiri tuone.
Kuna tetesi kwamba straika wao, Ibrahim Ajib naye anatakiwa na Yanga, tusubiri tuone.
Kumekuwa hakuna kauli nzuri zinazotolewa na baadhi ya
viongozi kuelekea kwa wachezaji wao.
Nakumbuka miezi kadhaa nyuma, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe alisikika kwenye vyombo vya habari akisema maneno ya shombo kwa kiungo wao, Mzimbabwe, Justice Majabvi ambaye kipindi hicho alikua akidai haki yake.
Nakumbuka miezi kadhaa nyuma, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe alisikika kwenye vyombo vya habari akisema maneno ya shombo kwa kiungo wao, Mzimbabwe, Justice Majabvi ambaye kipindi hicho alikua akidai haki yake.
Kwa uvumilivu aliokuwa nao Majabvi, akabaki na mpaka leo
anaendelea kuitumikia timu hiyo iliyopoteza nafasi kwa mara nyingine tena ya
kushiriki michuano ya kimataifa.
Huu ni msimu wa nne mfululizo Simba haijashiriki michuano ya kimtaiafa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), mashabiki wamekuwa wakiulaumu uongozi wa klabu yao lakini viongozi wamekuwa hawajifunzi kitu.
Wachezaji wengi wa Simba wameondoka klabuni hapo kwa mizengwe
na sitashangaa kuona wengine wakiondoka siku zijazo kwa staili kama ya Kessy.
Kessy alikuwa anataka kubaki Simba, lakini alipoanza
kudai maslahi zaidi, Simba kwa kuona haina ikataka kutumia ubabe wao
kumlazimisha kufanya wakitakacho, Kessy akagoma, kukaanza malumbano.
Katika malumbano hayo, siku moja Ofisa Habari wa Simba, Hajji Manara alinukuliwa na vyombo vya habari akisema: “Kessy hata akiondoka lakini Simba itabaki.
Simba ilikuwepo kabla yake kwani yeye ndiyo nani. Aende tu Simba si ya baba yake wala ya mama yake.”
Ni wazi inaonesha kwamba viongozi wa Simba wamekua
wakitumia ubabe wao kuiendesha timu, hali hiyo ni mbaya na inaweza kuleta hali
mbaya zaidi ndani ya Simba siku za usoni. Wataendelea kuboronga kwa kutojitambua.
Hakuna asiyefahamu kwamba ndani ya Simba kwa sasa hali
si nzuri, na hiyo ilianza kujitokeza mara tu walipotolewa kwenye michuano ya
Kombe la FA hatua ya robo fainali dhidi Coastal Union. Tumaini la kwanza la
kushiriki michuano ya kimataifa likaondoka.
Baada ya hapo wakaboronga katika michezo mitatu
mfululizo ya Ligi Kuu Bara na kutoka kileleni, wakawaacha Yanga wakikamata usukani
na mpaka wanatangazwa kuwa mabingwa hivi karibuni.
Watu wengi wamekuwa wakiizungumzia Simba kwa lugha
tofauti lakini lengo lao likiwa ni moja tu, kuwapa ushauri wa nini wanatakiwa
kufanya kuondokana na hiki kinachowatokea misimu nenda rudi.
Ni hivi karibuni tu lingine limeibuka klabuni hapo,
wachezaji wa kigeni waligoma wakidai mishahara yao, wakati wanagoma timu
ilikuwa na safari ya kwenda Ruvuma kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya
Majimaji.
Wachezaji wachache wakasafiri na kuwaacha wale ‘maproo’
wakiendelea na mgomo. Kesho yake wachezaji wawili kati ya hao ‘maproo’ ambao ni
Vincent Angban na Majabvi, wakaungana na timu.
Wengine waliobaki ambao ni Hamisi Kiiza, Juuko Murshid,
Emery Nimubona, Brian Majwega na Paul Kiongera, inasemekana hawatakiwi tena
klabu hapo.
Najiuliza hivi kama kweli hawa wote wakiondoka, Simba itakuwa inaonekanaje siku zijazo ukiangalia kwa sasa Kiiza na Juuko wanaonekana kuibeba zaidi timu hiyo.
Kiiza ndiye kinara wa mabao kwenye ligi kwa wachezaji wa Simba akiwa nayo 19. Juuko ndiye nguzo imara kwenye safu yao ya ulinzi.
Wakiondoka na kama hawatapatikana mbadala wao wa
uhakika, naiona Simba ikimaliza ligi msimu ujao ikiwa nje ya nafasi tano za juu.
mdosejr@gmail.com
mdosejr@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni