Arusha:Mtu mmoja afariki na 2 kukamatwa
Mtu mmoja amefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu mjini Arusha Tanzania.
Polisi wamewakamata wayu wawili wakihusishwa na
shambulio hilo lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian
cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni