STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 5 Julai 2014

AVEVA AMPUUZIA MBALI WAMBURA,

 

.
Aveva amempa 'makavu' Wambura  

RAIS wa klabu ya Simba, Evans Aveva, amesema kwamba hana muda wa kubishana na mtu yoyote kwasababu hali hiyo itaondoa shauku ya kuiandaa timu yao ili iwe na ubora na kuwapa raha mashabiki wake.
Kauli ya Aveva imekuja siku moja baada ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa Shirikisho la Soka la (TFF), Michael Wambura , kuibuka kuwatetea wanachama 69 waliosimamishwa uanachama kutokana na kuipeleka klabu yao Mahakamani, sambamba na kusema hataki kujadiliwa na Mkutano Mkuu
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Aveva alisema kuwa mambo yote yanaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Simba SC, hivyo hakuna sababu ya kuendelea kubishana na watu kupitia Vyombo vya habari.
Alisema kuwa kitendo cha kuendelea kutoleana matamko ni kuuminya muda wa kutafakari mambo muhimu yenye kuijenga klabu ya Simba, ambayo kwa miaka minne imeshindwa kuwapa raha wanachama na mashabiki wao kwa ujumla.
“Hii ni Simba mpya yenye kila sababu ya kufikia malengo yake, hivyo sioni kama wapo watu wanaotaka tuendelee kubishana kwenye vyombo vya habari wakati kanuni na sheria zinajieleza wazi juu ya wale wanaopeleka masuala ya soka mahakamani.
“Kutokana na kupania kuvunja makundi ndani ya Simba, pia nilitoa agizo la kuandaliwa kwa Mkutano Mkuu utakaokuwa na nia njema ya kujadili baadhi ya wanachama wake, akiwamo Wambura, sasa inashangaza kwanini hataki,” alisema Aveva.
Kwa mujibu wa Aveva, mwanachama yoyote anayekataa kujadiliwa kwenye Mkutano Mkuu huyo ana matatizo, maana Mkutano Mkuu ndio sehemu nzuri ya kujadiliana mambo yote yanayohusiana na klabu yao.
Aveva ameonyesha kuingia Simba akiwa na mipango lukuki ya kuipatia Simba mafanikio, huku akishirikiana na Kamati ya Utendaji, akiwamo Ally Suru, Collin Frish, Said Tully, Jasmin Costar na Idd Kajuna.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox