KAMATI
YA NIDHAMU ya FIFA inachunguza tukio ambalo lilisababisha Neymar
kuvunjwa Mfupa wa Mgongoni ili kuamua hatua dhidi ya Mchezaji wa
Colombia Juan Zuniga.
Beki huyo wa Colombia alimvaa Neymar na
kumgonga Mgongoni na Goti lake katika Dakika ya 88 ya Mechi ya Robo
Fainali ya Kombe la Dunia ambayo Brazil walishinda 2-1.
Mkuu wa Habari wa FIFA, Delia Fischer,
amesema: “Kamati ya Nidhamu inachunguza tukio hilo. Kucheza kwa Haki ni
kitu muhimu sana na tunataka kukwepa mambo magumu Uwanjani.”
Nae Ronaldo, Mchezaji wa zamani wa Brazil aliewahi kutwaa Kombe la Dunia, anaamini Zuniga alikusudia kumuumiza Neymar
.
.
Akiongea kwenye Mahojiano na Wanahabari,
Ronaldo alisema: “Alimvaa kwa nguvu mno, naamini Mchezaji yule wa
Colombia alikusudia kuumiza. Sidhani kama ni Mpira wa kawaida ule. Sijui
kama alipanga tangu mwanzo kufanya vile lakini naamini alitumia nguvu
kubwa kumvamia!”
Zuniga amejitetea kwamba hakukusudia
kumuumiza Neymar na amesema: “Ni mchezo wa kawaida, sikukusudia
kumuumiza Mchezaji. Nilikuwa Uwanjani, nikicheza kwa ajili ya Jezi ya
Nchi yangu, si kuumiza Mtu. Nilikuwa nikitetea Jezi yangu!”
Kwenye Fainali hizi za Kombe la Dunia
huko Brazil, FIFA tayari ishatwanga Rungu lake kali kwa kumfungia Miezi
Minne Straika wa Uruguay Luis Suarez kwa kumuuma Meno Beki wa Italy
Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya KUNDI D kati ya Uruguay na Italy.
Mbali ya Miezi Minne ambayo haruhusiwi
kushughulika na chochote kuhusu Soka ikiwa ni pamoja na kufanya Mazoezi
na kukanyaga Uwanjani, Suarez pia amefungiwa Mechi 9 kuichezea Uruguay
na kudungwa Faini Dola 111,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni