KLABU KOSOVO YATAKA KUMSAINI SUAREZ AICHEZEE WAKATI WA KIFUNGO CHAKE!
KUOMBA
RADHI kwa Luis Suarez kwa kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini
wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia huko Brazil kati ya Uruguay na Italy
kumeonyesha ni ‘Mnyenyekevu’ kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa
Barcelona Andoni Zubizarreta
.
Inaaminika Suarez ndio mlengwa mkubwa wa
Barcelona kwa Wachezaji wanaotaka kuwanunua kabla Msimu mpya kuanza
licha ya Mchezaji huyo kuwa kwenye Kifungo cha FIFA cha Miezi Minne kwa
kumuuma Meno Chiellini.
Suarez, ambae awali alikana kumng’ata
Chiellini, Jumatatu alimuomba radhi Chiellini na Ulimwengu wa Soka bila
kuitaja Liverpool na hilo limechukuliwa kuashiria nia yake kuihama
Anfield.
Baadhi ya Wachambuzi wamedai Barcelona
ndio ilimshauri na kumhimiza Suarez kuomba radhi na uamuzi wa
Zubizarreta wa kuzungumzia uombaji radhi wa Suarez unaonyesha nia ya
Barcelona kumsafisha.
Zubizarreta alisema: “Suarez ameonyesha
ni mnyenyekevu kiasi cha kuomba radhi kwa kosa lake na hilo ni muhimu.
Amekuwa mnyenyekevu mkubwa kuwaomba radhi aliowadhuru. Kwa hili, huo ni
uamuzi mzuri amefanya!”
Aliongeza: “Kila Mtu anajua Luis ni Mchezaji Bora na kila Mtu anajua ni Mchezaji wa Liverpool.”
Zubizarreta aliongea hayo kuhusu Suarez wakati wa sherehe za kumtambulisha Mchezaji mpya alesainiwa na Barcelona Ivan Rakitic.
KLABU KOSOVO YATAKA KUMSAINI SUAREZ AICHEZEE WAKATI WA KIFUNGO CHAKE!
KLABU inayocheza Ligi Kuu huko Kosovo
inataka kumsaini kwa Mkopo Straika wa Liverpool Luis Suarez ambae
amefungiwa Miezi Minne kwa kumng’ata Meno Beki wa Italy Giorgio
Chiellini.
Klabu hiyo, Hajvalia, imetangaza kuwa
kwa vile Nchi yao na wao si Wanachama wa FIFA na hawatambuliwi nao
wanaweza kumtumia Suarez kuwachezea wakati yuko Kifungoni.
Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu hiyo,
Xhavit Pacolli, amesema: “Kwa vile sisi si sehemu ya FIFA, nadhani
anaweza kucheza kwetu. Tunayo Ofa tutaituma Liverpool. Akikubali kuja na
kucheza kwetu, tutamkaribisha. Hii itamsaidia sana yeye.”
Hivi sasa Suarez anahusishwa sana na
kuhamia Barcelona ambao wako tayari kutoa Dau la Pauni Milioni 80
kumnunua lakini Klabu hiyo ya Kosovo imesema itatoa Dau la Uhamisho wa
Mkopo la Pauni 25,000 na Mshahara wa Pauni 400 kwa Wiki.
Pacolli amesema: “Hiyo ndio Ofa yetu. Pengine inaonekana upuuzi kwake, lakini hiyo ndio tunaweza kutoa!”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni