STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 31 Julai 2014

HATIMAYE NEYMAR AANIKA SIKU YA KURUDI UWANJANI

Neymar reveals return date

NEYMAR ameweka wazi kuwa atarudi uwanjani agosti 18 mwaka huu kuitumikia Barcelona katika mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu ya kombe la Joan Gamper dhidi ya Leon.
 
Mbrazil huyo alivunjika mfupa wa uti wa mgongo wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia na alizikosa mechi mbili.
Neymar aliwakosa Ujerumani, hatua ya nusu fainali na Uholanzi mechi ya mshindi wa tatu.
 
Hata hivyo anatarajia kujiunga na Barcelona katika maandalizi ya msimu Agosti 5 mwaka huu na ataweza kucheza kwenye mechi ya Gamper ndani ya dimba la Camp Nou.
 
“Naimarika taratibu kutokana na majeruhi. Nitarudi Barcelona kwa asilimia 100,” aliwaambia waandishi wa habari nchini Brazil.
“Nahitaji kuwa na msimu mzuri na naangalia mbele kuwasaidia wachezaji wenzangu kupata matokeo mazuri. Pia nahitaji kuisaidia timu ya Brazil.

“Nina imani ya kucheza mechi ya Gamper Agosti 18.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox