Onyo mapema: Diego Costa akisherehekea baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza Uwanja wa Stamford Bridge
MABAO
ya mawili ya mapema kipindi cha kwanza ya Diego Costa yameipa Chelsea
ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Sociedad ya Hispania katika mchezo wa
kirafiki kujiandaa na msimu.
Akicheza
kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge tangu aiongoze timu
yake ya zamani, Atletico Madrid kuifunga timu ya Jose Mourinho katika
Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Costa alihitaji dakika nane tu
kuiteketeza Real Sociedad.
Alifunga
dakika ya kwanza na saba na sasa anafikisha jumla ya mabao manne
aliyoifungia Chelsea tangu ajiunge nato akitokea Atletico mwezi
uliopita.
Kikosi
cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic/Zouma dk82, Cahill/Azpilicueta
dk45, Terry/Christiansen dk86, Ake/Luis dk45,Ramires/Oscar dk45,
Matic/Van Ginkel dk82, Fabregas/Mikel dk71, Schurrle/Willian dk45,
Costa/Torres dk60 na Hazard/Salah dk82.
Real
Sociedad: Zubikarai, Zaldua/C. MartÃnez dk59, Ansotegi/Mikel dk11,
Inigo Martinez, De la Bella/Yuri dk72, Markel/Elustondo dk59,
R.Pardo/A.Oyarzun dk72, Granero/Chory dk65, X.Prieto/HervÃas dk72,
Canales/Hernandez dk72 na Agirretxe/Estrada dk65.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni