STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 3 Agosti 2014

KABURU BILA KUMUNG`UNYA MANENO ACHANA HADHARANI KUFUKUZWA KWA RICHARD WAMBURA


RASMI wanachama wa klabu ya Simba sc wapatao 680 wamelazimika kuwafuta uanachama wanachama wenzao 72 waliokwenda mahakamani akiwemo mgombea aliyeenguliwa katika uchaguzi uliopita, ‘Kidume’ Michael Richard Wambura.
Maamuzi hayo yemefikiwa katika mkutano mkuu wa kawaida wa klabu ya Simba uliofanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam.
Mbali na wanachama kujadili masuala muhimu na kupokea taarifa mbalimbali za klabu katika mkutano huo, Agenda ya wanachama 72 waliokwenda mahakamani ndio ilibebea uzito wa juu zaidi na kila mtu alikuwa na hamu ya kutaka kujua nini hatima ya Wambura na wenzake.
Wambura aliipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 na suala hilo lilisababisha kuenguliwa kwa jina lake katika uchaguzi mkuu wa Simba na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu'

Lakini alikata rufani katika kamati ya Rufani ya shirikisho la soka Tanzania TFF, chini ya mwenyekiti wake, Jaji Julius Mutabazi Lugaziya na kushinda, hivyo kurejeshwa kwenye mchakato.
Sababu kubwa kumrudisha ilikuwa ni kwamba, tangu Simba itangaze kumsimamisha uanachama Wambura mwaka 2010, ilimuacha huru na kuendelea kushiriki shughuli za klabu kama mwanachama hai ikiwemo kulipia ada ya kadi yake ya uanachama.
Lakini kamati ya Ndumbaro ilimuengua tena kwasababu ya kupiga kampeni kabla ya muda.
Kutokana na nguvu kubwa aliyonayo Wambura,watu walisubiri kujua nini itakuwa hatima yake leo hii.
Mtandao huu umezungumza na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye amethibitisha kufutwa uanachama wanachama 72 pamoja na Wambura.
“Kikao kilikuwa kizuri na kimeendeshwa na Rais wetu Bwana Evans Aveva. Wanachama wamepata nafasi ya kujadili masuala ya msingi na wamepokea taarifa mbalimbali, lakini vilevile kuna maamuzi ambayo yalifanyika,” alisema Kaburu.
Michael Richard Wambura amefukuzwa uanachama TFF

“Kulikuwa na agenda kubwa ambayo ilibeba uzito mkubwa sana katika kikao cha leo ni ile ya wanachama 71 waliokwenda mahakamani.
“Ikimbukwe kuwa mwaka 2010, Bwana Michael Richard Wambura na Bwana Nchemi walikwenda mahakamani na hadi sasa walikuwa hawajawi kuzungumza kwenye mkutano mkuu.”
“Vilevile katika mkutano mkuu wa 2014, kuna wanachama 70 waliokwenda mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi, kwahiyo leo kwa kauli moja wanachama wa klabu ya Simba wapatao 680 waliohudhuria kikao wamelaizimika kuwafuta wanachama hao waliokwenda mahakamani”

“Kitendo walichofanya ni utovu wa nidhamu, kwa mujibu wa katiba ya klabu yetu ya Simba, ibara ya 55 inasema mwanachama anayekwenda mahakamani basi afutwe uanachama wake”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox