Real Madrid imekubali kumuachia Angelo Di Maria ambaye anatua Man United
kw akitita cha pauni milioni 64.
Uhamisho wake utavunja rekodi na kuwa ghali zaidi England ukiupita ule
wa pauni milioni 50 wakati Fernando Torred alipotua Chelsea akitokea Liverpool.
Di Maria raia wa Argentina, anatarajia kutua jijini Manchester leo kwa
ajili ya vipimo na kumalizana na wenyeji wake.
Kocha Carlo Ancelotti wa Madrid amethibitisha kwamba mkali huyo
alikwenda kuwaaga mazoezini kwamba anaondoka.
Man United imekuwa ikifanya juhudi kujiimarisha baada ya kusuasua kwa
msimu mzima na pia kuanza vibaya msimu mpya kwa kipigo na sare dhidi ya Swansea
na Sunderland.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni