STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 11 Agosti 2014

PATRICK PHIRI NDIYE ATAKUWA KOCHA MPYA SIMBA




Simba iko katika hatua nzuri ya mazungumzo na Patrick Phiri na huenda akatua nchini ndani ya siku tatu kuanza kazi.
Phiri raia wa Zambia anatarajia kutua nchini kuchukua nafasi iliyoachwa na Zdravko Logarusic ambaye ametimuliwa na uongozi wa Simba baada ya kutoridhika namwenendo wake
.
Logarusic raia wa Croatia anatarajia kuondoka nchini kurejea kwao na Phiri aliyewahi kuinoa Simba kwa vipindi vitatu tofauti, yuko katika hatua za mwisho kutua nchini.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, makocha kadhaa wametuma wasifu wao kuwania kazi ya Loga.
Lakini uongozi wa Simba uliwaingiza fainali Phiri na Milovan Cirkovic lakini Mzambia akaonekana kukubalika na wajumbe wengi wa kamati ya utendaji.
“Mjadala ulianza baada ya kuona Loga ataondoka, mara moja Phiri amepata nafasi ya kwanza baada ya kumzidi Milovan na amekubali kuja, kuna mambo madogo ya kumalizia,” kilieleza chanzo.
“Lakini kuna mambo madogo ya kumalizia na yakikubalika, Ijumaa au Jumamosi atakuwa Dar kuungana na Matola ambaye anakuwa bosi kwa muda.”
Phiri ni kati ya kocha kipenzi cha Wanasimba na amekuwa akikubalika kutokana na kazi yake nzuri. Amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Zambia ‘Chipolopolo’ aliyoipeleka hadi Kombe la Mataifa Afrika iliyofanyika nchini Ghana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox