STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 11 Agosti 2014

SIMBA SC YAWAPA MIKATABA YA MIAKA MIWILI KILA MMOJA , KWIZERA NA KIONGERA... WAKAMILISHA IDADI YA WACHEZAJI WA 5


Wanaungana tena; Paul Kiongera alicheza pamoja na Donald Mosoti Gor Mahia ya Kenya

SIKU moja baada ya kuvunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic, Simba SC imewasainisha mikataba ya miaka miwili kila mmoja, kiungo Pierre Kwizera raia wa Burundi na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera.
Simba SC jana ilivunja mkataba na Loga ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakaimu Ukocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.
Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.
Wawili hao wanakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni katika klabu hiyo kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiungana na mabeki Mganda Joseph Owino, Mkenya Donald Mosoti na mshambuliaji Mrundi, Amisi Tambwe.
Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox