STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 29 Agosti 2014

RONALDO AMTABIRIA MAFANIKIO DI MARIA AKIWA UNITED.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amemtabiria mafanikio mchezaji mwenzake wa zamani Angel Di Maria katika klabu yake mpya ya Manchester United. 
 
Nyota huyo wa kimataifa wa argentina alifanikiwa kukamilisha usajili uliovunja rekodi nchini Uingereza Jumanne iliyopita baada ya kushindwa kufiti katika kikosi cha Carlo Ancelotti huku akipewa jezi namba saba ambayo imewahi kutimiwa na Ronaldo wakati akiwa United
 
Ronaldo ambaye alicheza misimu sita na United, anaamini kuwa uhamisho huo ndio Di Maria aliokuwa akihitaji na ana uhakika nyota huyo anaweza kuisaidia timu hiyo kubadili mwelekeo baada ya kuanza vibaya msimu mpya wa Ligi Kuu. Akihojiwa Ronaldo ambaye jana ametunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya katika sherehe zilizofanyika jijini Monaco, amesema Di Maria kwenda United ni jambo ambalo litamsaidia kwani anaamini amekwenda katika moja ya klabu bora duniani hivyo anamtakia mafanikio akiwa huko. Ronaldo aliendelea kudai kuwa amezungumza naye na kumwambia kuwa jezi namba aliyopewa ina majukumu makubwa lakini anadhani ataitendea haki jezi hiyo kwani ni mchezaji mahiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox