Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Septemba 5 nchini Morocco.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine amesema
wamepokea mwaliko na tayari Kocha Mart Nooij ameishatangaza kikosi
chake.
"Ni
tarehe ambayo iko ndani ya tarehe za Fifa, hivyo maandalizi yanaanza na
kocha ameishaita kikosi," alisema Mwesigwa ambaye pia ni katibu mkuu wa
zamani wa Yanga.
Katika
mechi yake ya mwisho, Stars ilichapwa kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini
nchini Msumbuji na kutolewa katika mbio za kuwania kucheza michuano ya
Mataifa Afrika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni