STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 5 Agosti 2014

TAARIFA YA POLISI KUHUSU ISMAIL ADEN RAGE KUNUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI


Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, amenusurika kifo na kuumia bega la Kushoto akiwa na watu wengine watatu baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya Toyota Lund Cruser T 845 DQS (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la Chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini Dodoma kuanza vikao vya Bunge la Katiba hapo kesho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime, amesema ajali hiyo imetokea leo Agost 4, 2014 na kuwa imetokea katika eneo la Njia panda ya Kigwe katika barabara ya Singida Dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge Maalum la katiba.
Amesema Rage, ameumia katika bega la kushoto na mgongoni huku Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora, Munde Abdalla Tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Amesema watu wengine waliokuwepo katika gari hilo ni pamoja na Mwanahamis Athumani, John Hoya ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Hata hivyo amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox