STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 5 Agosti 2014

EXCLUSIVE: LIGU KUU KUTANGAZA MASHINDANO MAPYA YA ULAYA KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 21


Winners: Chelsea celebrating victory in the 2013/14 U21 Premier League
Mabingwa: Chelsea wakishangilia kombe la vijana chini ya miaka 21 kutoka timu za ligi kuu msimu wa 2013/14 
 
MSIMU huu uongozi wa ligi kuu unatarajia kuzindua mashindano mapya ya kombe la ulaya kwa timu za ligi kuu nchini England chini ya miaka 21 na timu kutoka nje ya England.
Vikosi vya vijana chini ya miaka 21 kutoka timu nane (8) za juu katika msimamo wa ligi kuu Engalnd  zikiwemo klabu za Manchester City, Manchester United  na Chelsea vitashiriki pamoja na timu nane (8) kutoka nje ya England ambapo jumla ya timu itakuwa ni 16.
Hii hatua ni kutekeleza mkakati maalumu wa soka la vijana ulioanzishwa mwaka 2011 ili kuwaimarisha vijana wanaozalishwa na klabu za juu za England.
 

TIMU 16 ZITAKAZOSHIRIKI 

Timu za England: Chelsea, Fulham, Leicester City, Man City, Man Utd, Southampton, Sunderland, West Ham.

Timu za Ulaya: Celtic, Athletic Bilbao, Benfica, Borussia Monchengladbach, Schalke, FC Porto, PSV Eindhoven, Villarreal
Liverpool, walioshiriki ligi ya vijana chini ya miaka 21 msimu uliopita hawatashiriki mashindano hayo na badala yake nafasi hiyo imeenda kwa West Ham waliomaliza nafasi ya tisa katika msimamo msimu uliopita.
Mashindano hayo yataenda sambamba na ligi ya vijana chini ya miaka 21. 
Kwa sasa yatawavutia watu wengi zaidi kwasababu Sky Sports na BT Sports watarusha 'Laivu' mechi 10.
Waandaaji wana matumaini kuwa michuano hii itawavutia watu wengi na timu zitapata wachezaji wao wazuri ili kuwaingia katika timu za wakubwa.
Mkurugenzi wa akademi ya Schalke ,Oliver Ruhnert  alisaidia kuzalisha wachezaji wanne walioisadia Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka huu na timu yake itashiriki michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 21.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox