TIMU ya taifa ya
wanawake ya Ujerumani imefanikiwa kunyakuwa Kombe la Dunia kwa wachezaji
wanawake wenye umri chini ya miaka 20 kwenye michuano iliyokuwa
inafanyika huko Montreal, Canada.
Ujerumani walifanikiwa kuwazidi
maarifa Nigeria katika mchezo wa fainali kwa kuwafunga bao 1-0 kama
ilivyokuwa kwa timu ya wanaume iliyonyakuwa taji hilo katika michuano
iliyofanyika nchini Brazil.
Pamoja na kuonyesha mchezo mzuri huku
wakimiliki vyema mpira, Nigeria walishindwa kabisa kupenya ngome ngumu
ya wapinzania wao. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Lena
Petermann ambaye alifunga katika dakika ya nane ya muda wa nyongeza
baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika muda wa
kawaida. Mshambuliaji wa Nigeria na mfunmgaji bora wa mashindano hayo
Asisat Oshoala alikosa nafasi kadhaa za wazi wakati golikipa wa
Ujerumani Meike Kamper alitajwa kama mchezaji bora wa mechi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni