PAMOJA na mchezo
kuchezwa katika Uwanja wa Wembley, nyumba ya soka la Uingereza ni
wachezaji watatu pekee wa Uingereza walioanza katika mchezo wa Ngao ya
Hisani kati ya Arsenal na Manchester City. Wachezaji wote watatu wa
Uingereza waliocheza walikuwa ni wa Arsenal wakiwemo mabeki Kieran Gibbs
na Calum Chambers na kiungo Jack Wilshere huku Alex Oxlade-Chamberlain
akitokea benchi.
Mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City hawakuanzisha
mchezaji hata mmoja wa Uingereza ambapo wote walianzia benchi akiwemo
kipa Joe Hart, Micah Richards, James Milner na Scott Sinclair.
Mwaka
uliopita wachezaji 10 wa Uingereza walianza katika mchezo wa Ngao ya
Jamii uliokutanisha timu za Manchester United na Wigan Athletic huku
mwaka mmoja kabla ya huo wachezaji wanne pekee walianza katika mchezo
kati ya Manchester City na Chelsea.
Wadau mbalimbali wa soka nchini humo
wamekuwa wakilalamika kutumika kwa wachezaji wa kigeni katika timu
kubwa au Big Four akiwemo kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uingereza
Gary Neville. Neville amesema wamekuwa wakijimaliza taratibu kwani
wamekuwa wakiwacheza Scotland na Jamhuri ya Ireland wakati wao wenyewe
wanaelekea hukohuko. Neville aliendelea kudai kuwa miaka 25 iliyopita
ilikuwa huwezi kukosa wachezaji kutoka Scotland au Jamhuri ya Ireland
katika timu kubwa kama Liverpool na Manchester United lakini hivi sasa
hakuna hata mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni