STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 7 Septemba 2014

DI MARIA APASUA BOMU: REAL MADRID WALINITUMIA BARUA KUNIZUIA KUCHEZA FAINALI KOMBE LA DUNIA

 
Di Maria amesema Real Madrid walimzuia kucheza Fainali Kombe la Dunia
WINGA Angel di Maria amesema Real Madrid ilimuamrisha asicheze mechi ya Fainali Kombe la Dunia. 
Mchezaji huyo mpya wa Manchester United aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 60, dau la rekodi kwenye soka ya Uingereza, tayari amemtupia lawama Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwa kuondoka kwake kwa mabingwa hao wa Ulaya, akisema hakuwa na nia ya kuondoka.
Di Maria alikuwa shakani kuichezea Argentina katika Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani Julai mwaka huu kwa sababu ya majeruhi, na ameweka wazi  kwamba uamuzi wa kutocheza mechi hiyo ulichukuliwa na kocha Mkuu wa Argentina, Alejandro Sabella, na si Madrid ambao walimtumia barua kumshauri asicheze."Nachopenda zaidi ni kuichezea Argentina,"amesema Di Maria. "Nilipokea barua Saa 5:00 asubuhi kutoka Real Madrid, katika siku ya mchezo wakati nikiwa na daktari wa viungo, akijaribu kufanya jitihada za kuniwezesha kucheza fainali, ikiniambia nisicheze fainali ya Kombe la Dunia. 
Nilikuwa nafikiria kucheza fainali, na pia nilijua kwamba iwapo ningefanya hivyo kulikuwa kuna asilimia 90 za kuumia tena. Nilipoisoma, nikaichana barua. Nilipata maumivu sana asubuhi ile. Hicho ni kitu kibaya zaidi kuwahi kunitokea maishani. Sikuzungumza na mtu yeyote katika klabu juu ya hili. Haijalishi. Mwishowe, alikuwa ni Sabella aliyefanya maamuzi na ilikuwa ni kwa nia nzuri," amesema.
Akizungumza na kipindi cha Redio ya Argentina, America y Closs, Di Maria amesema: "Nilizungumza na Alejandro na ulikuwa uamuzi wake. Sikutaka kumpa shinikizo. Nilijua ningeweza kutoka née baada ya dakika 15 na kuiacha timu, sikutaka hivyo," ameongeza.' 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox