STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 11 Septemba 2014

MWANARIADHA PISTORIUS AFUTIWA MASHITAKA YA MAUAJI, ILA ANASUBIRI KESI NYINGINE

Mwanariadha maarufu mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius  amefutiwa mashitaka ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp.

Pistorius kupitia mlango wa choo alimlipiga mwanamitindo huyo risasi nne zilizotoa uhai wake lakini akasema alidhani wameingiliwa na mpenzi wake alikuwa chumbani kwao.
Lakini jaji Thokozile Masipa aliyekuwa anaendesha kesi hiyo kwenye mahakama ya Pretoria, Afrika Kusini amemfutia mashitaka ya mauaji kwa madai upande wa ushahidi haukutoa vilelezo vilivyojitosheleza.
Akisoma hukumu yenye kurasa 3,000 Jaji Masipa alisema mwanariadha huyo angeweza kupatikana na hatia kama ushahidi ungejitosheleza.
Alisema kutokana na ushahidi wa kila upande inaonekana mwanariadha huyo hakukusudia kwa kuwa alijaribu kujilinda.
Hata hivyo bado Pistorius atalazimika kusubiri kipande kingine cha kesi hiyo kuhusiana na kifo hicho.

Hivyo kimsingi kuna kesi ambayo itaendelea kusikilizwa baada ya yeye kuonekana hana hatia ya mauaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox