STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 3 Septemba 2014

NMB WASAINI MKATABA WA KUIDHAMINI AZAM FC MIAKA MIWILI

Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad akiwa akipokea jezi mpya za klabu hiyo kutoka kwa wadhamini, NBM leo Chamazi

BENKI ya NMB imeingia mkataba wa udhamini wa miaka miwili na klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Azam FC ambao utahusu gharama za usafiri na baadhi za uendeshaji wa timu.
Akizungumza leo makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Azam FC Sheikh Said Muhammad Said amesema kwamba mkataba huo unaanza mara moja.
Sheikh Said amesema kwamba wanaishukuru NMB kwa kuwapa Mkataba huo na anaamini utaongeza ufanisi katika klabu yao. “Tumeupokea kwa furaha Mkataba huu na tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa NMB kwa kuungana nasi,”amesemaAkifafanua kuhusu Mkataba huo, Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Iddrisa Mohammed ‘Father’ amesema NMB itanufaika kwa kutangazwa kwenye jezi za Azam, mabasi na pia kuweka mabango yao kwenye Uwanja wa Azam Complex.

“Nembo za NMB zitapamba jezi za Azam FC kuanzia mazoezini na kwenye mashindano yote, vyombo vyetu vya usaifiri kadhalika vitawekwa nembo za NMB kama itakavyokuwa kwenye Uwanja wetu a Azam Complex,”amesema Father.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Mark Wiessing amesema mafanikio ya Azam FC ndiyo yaliyowavutia kuingia nao ndoa hiyo. “Mafanikio ya Azam FC katika soka ya Tanzania ndiyo yametuvuta kuingia nao ushirika huu,”amesema.
Azam FC inakuwa timu ya pili kihistoria nchini kuingia mkataba wa udhamini na taasisi ya kifedha, baada ya Simba SC mwaka 2003, ambao walifunga ndoa na NBC, ambayo hata hivyo ilivunjika mwaka 2004.
Azam FC na NMB wakitiliana saini Mkataba huo 


Aidha, NMB anakuwa mdhamini wa kwanza wa klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabishara Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake tangu imeanzishwa mwaka 2004 kabla ya kupanda Ligi Kuu mwaka 2008.
Tangu imeanzishwa, Azam FC imekuwa ikitangaza bidhaa zinazotengezwa na kampuni ya Bakhresa pekee. NMB imewahi kuidhamini timu ya taifa, Taifa Stars kati ya mwaka 2007 na 2010. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox