STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 7 Septemba 2014

PATRICK PHIRI SASA SIMBA RAHA TUPU! ANGALIA WALIVYONOGA JANA KWENYE PICHA KIBAO

Wachezaji wa Simba sc wakishangilia bao la Ramadhan Singano 'Messi'  jana Simba ikiitandika Gor Mahia 3-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

ZAMANI mtu anayeitwa Baba katika familia alikuwa mtu wa kuogopwa na watoto na pengine hata mke wake wa ndoa.
Kutokana na ufalme huo, akina Baba walikuwa wanatamba na kuvimba kichwa pale wanapoogopwa na wakigundua watoto hawana uogo kwao, walidhani hawaheshimiwe.
Baba anaporudi nyumbani kutoka matembezini, watoto hukimbia kwenda kulala mara wasikiapo sauti yake nje.
Baadhi ya watu walidhani kuwa ukali ni njia mojawapo ya kulea familia katika ubora, lakini walio wengi walishindwa kufikia malengo kwasababu watoto wao walishindwa kuwa huru.
Kuwa mkali sana pale mtoto anapofeli mtihani sio suluhisho la kumfanya afaulu. Hakuna kitu kibaya kama kufanya kitu ukiwa katika usimamizi mkali au hofu ya kufeli.
Kama upo kwenye chumba cha mtihani na unawaza jinsi baba atakavyokuchapa ukifeli, basi utakuwa na presha ya mtihani na utashindwa kufanya vizuri.
Kufeli na kufaulu kupo kwa ajili ya wanafunzi, hutakiwa kuwaza kufaulu tu wakati kufeli pia kupo.
‘Udingi’ ni tatizo kubwa sana hasa ulimwengu huu wa utandawazi. Siku hizi U-baba bora unaopendwa na watoto ni kuwa mpole na kujua namna ya kuzungumza nao pale wanapokosea.
Busara ikitawala katika mazungumzo yako, basi una asilimia kubwa ya kuwavutia watoto wako na wakafanya kile unachotaka.
Hata katika mpira wa miguu, zamani makocha wengi walikuwa wanaendekeza ‘udingi’. Kuwashauri ilikuwa ngumu na uhusiano na wachezaji ulikuwa wa Baba na mtoto.
Mfano aliyekuwa kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari ana ‘udingi’ mwingi. Hashauriki, haambiliki na hata wachezaji wake wanamuogopa kwasababu hajajirahisisha kwao.
Kutokana na tabia hii, Scolari amejikuta akifeli katika soka la kisasa. Siku hizi makocha wanaofanikiwa ni wale wenye mahusiano na wachezaji kama ‘washikaji’.
Emmanuel Okwi alikuwa chachu ya mabao ya Simba jana

Ikitokea tatizo wanalitatua kirafiki tu, na wakati mwingine mchezaji anamchukulia kocha wake kama jamaa yake tu. Anakuwa na uhuru wa kuomba kitu, kushauri kitu na hata kueleza mambo yake binafsi.
Makocha wanakuwa kama walezi na wanawapanga wachezaji kisaikolojia. Kutokana na hili wachezaji wanajikuta ni marafiki wa makocha wao na kazi inafanyika vizuri.
Kuna aina ya makocha huwa ni wakali kupindukia. Hataki kuona mchezaji anakosea, lakini wanajisahau kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa.
Mfano ni aliyekuwa kocha wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic maarufu kama Loga. Huyu jamaa kama ulibahatika kumuona katika mazoezi yake na hata wakati wa mechi, alikuwa hana uvumilivu, na ukali wake uliwafanya wachezaji wawe wanyonge mno.
Mchezaji anaingia uwanjani, lakini fikira zake zote zipo katika kukwepa makosa.
Unaweza kuona Ramadhani Singano ‘Messi’, Amiss Tambwe yuko nafasi nzuri ya kufunga na anatakiwa kujaribu kupiga shuti, lakini anatafuta sehemu ya kupeleka mpira kwasababu sababu anaogopa kumuudhi Loga.
Ukikosea muda huo huo unakwenda kukalia ‘benchi’ a.k.a gogo.Lakini kumbe mpira hauko hivyo, hutakiwa kuogopa kukosea, fanya ufikiriavyo, ukikosea ni sehemu ya mchezo wa soka.
Baada ya mazingira hayo magumu kwa wachezaji wa Simba, uongozi ukasikiliza kero zao za chini kwa chini na kuamua kuachana na Loga aliyedaiwa kuwatukana Amri Kiemba, Shaaban Kisiga na wengineo baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco United ya Zambia katika mechi ya Tamasha la ‘Simba Day’, Agosti 9 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Mzambia Patrick Phiri alichukua mikoba na kwa mara ya kwanza jana ameiongoza Simba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Simba ilishinda mabao 3-0 ambapo Mkenya Paul Kiongera alifunga mawili na Ramadhani Singano ‘Messi’ alishindilia moja.
Mafanikio?: Aliyekuwa kocha wa Simba, Logarusic aliwafunga Yanga mabao 3-1 na kutwaa kombe la Nani Mtani Jembe mwezi desemba kwa jana uwanja wa Taifa.

Wakati mashabiki wakifurahia ushindi huo, binafsi nilikuwa nawatazama wachezaji wa Simba kwa jicho la tatu na nilibaini baadhi ya mambo ya msingi kuongezeka kwao.
Mosi; lugha ya miili yao ‘Body language’ ilionesha kuwa wapo huru kucheza mpira. Walikuwa wapesi na kufanya kila wanachotaka tofauti na kipindi cha Loga.
Wachezaji kama ‘Messi’, Kiongera, Uhuru Seleman, Shaaban Kisiga walionekana kuonana vizuri na mawasiliano yao yalikuwa mazuri.  Hawakuonekana kuwa na hofu ya kukosea, walicheza kwa kujiamini, kwa uhuru na ilisaidia sana kuifanya Simba iwe na makali kipindi cha pili.
Kipindi cha Loga wachezaji hawakuwa na uhuru, hofu ilitanda na walishindwa kutumia tafsiri za akili zao katika kuucheza mpira. Muda wote waliwaza maelekezo ya mwalimu.
Katika mpira maelekezo ya kocha ndio hutumika kucheza mpira,lakini kuna mazingira inakulazimu kutumia akili yako. Na ndicho kilionekana kwa wachezaji wa Simba.
Pili; ladha ya mpira wa Simba ilionekana. Kwa kawaida Watanzania wengi wanapenda sana kuona mpira wa pasi ‘passing football’. Na huo ndio utamaduni wa Simba kwa muda mrefu.
Kocha mkuu wa Simba sc, Patrick Phiri

Simba wana utamaduni wa kuweka mpira chini na kupiga pasi fupi fupi, lakini kwa muda mrefu mpira wa aina hiyo ulipotea. Lakini kurejea kwa Phiri kumeonekana kuwa chachu ya kurudi kwa mpira huu.
Wachezaji hasa kipindi cha pili walicheza vizuri kuanzia katikati na walionana kwa pasi zilizosisimua mashabiki wa Simba.
Tatu; wachezaji wanaonekana kumridhia Phiri. Kocha huyu ni kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Simba. Historia yake ni kubwa Msimbazi. Mara baada ya kurudi tena kwa mara ya tatu, wachezaji walionekana kumkubali na wengine kuonesha furaha yao kwa kujaribu kumueleza kero walizokuwa nazo.
Phiri ni mtu mzima, lakini hana ‘udingi’. Anapenda sana kuzungumza na wachezaji na siku zote huwafanya kuwa marafiki zake. Hana ukali usiokuwa na sababu. Ni mwalimu anayependa zaidi kuelekeza kuliko kufoka.
Huwa anayakubali makosa na ana amini ni sehemu ya mchezo. Na ndio maana wachezaji wanapasiana kwa uhuru, wanacheza kwa kuonesha vipaji binafsi na kucheza kitimu. Simba walionekana kuwa na ushirikiano mzuri kuanzia nyuma mpaka mbele.
Viungo walicheza vizuri na kuipandisha timu na hatimaye kutengeneza nafasi za kufunga.
Unaweza kusema Gor Mahia hawana ukali kwa sasa, lakini nadhani ilikuwa muhimu kuangalia namna Simba walivyocheza vizuri.
Nne; mashabiki wa Simba wameonekana kujenga imani katika timu yao. Kama una kumbukumbu nzuri, msimu uliopita, hususani mechi za mwishoni katika mzunguko wa pili, mapato ya mlangoni kwa Simba yalipungua mno.
Kuna wakati mapato ya jumla yalikuwa milioni 20 tu. Haikuwa kawaida kwa timu kubwa kama Simba, lakini ililazimika kuwa hivi kutokana na mashabiki wengi kuisusa timu ya Loga.
Wachezaji walionekana kucheza chini ya kiwango na ilitafsiriwa kama ni kumgomea Loga. Dhahiri, kocha huyu hakupendwa. Mashabiki hawakwenda uwanjani kwa wingi, wakati wa Yanga waliendelea kumiminika.
Lakini kama ulikuwepo jana uwanjani, mashabiki walifurika kwa wingi ukizingatia ni mechi ya kirafiki. Walionekana kuwa na imani kubwa na Phiri na walishangilia kwa muda wote wa mechi na kuwakera wenzao wa upande wa pili.
Nadhani nguvu na uumoja umerejea simba na hii itawasaidia kufanya vizuri uwanjani. Cha msingi, wana Simba wote wanatakiwa kumuamini kocha na wachezaji wake. Wampe muda ili afanye kazi yake.
Phiri ni Simba, Phiri ni kocha sahihi kwa Simba kwasababu ni mwenyeji Msimbazi na anaijua Simba vizuri mno. Simba ni kama nyumbani kwake, na ndio maana unaona timu inarudi kwa muda mfupi baada ya kushika hatamu. Sijui nini kitatokea baadaye, lakini kwa kiwango cha jana ‘Well done’ Simba Sports Club.

Jumapili njema!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox