Neymar amekuwa akitazamwa kama mkombozi wa Brazil na atabeba matumaini ya taifa
NEYMAR atakuwa nahodha wa Brazil katika
mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Colombia na amepewa baraka zote na
kocha wa timu hiyo, Dunga.
Thiago Silva, ambaye alikuwa nahodha
chini ya kocha aliyetimuliwa, Luis Felipe Scolari hayupo kikosini na
hatacheza mechi za kirafiki za raundi hii kutokana na majeruhi.
Neymar mwenye miaka 22 atakuwa nahodha
mdogo zaidi kuiongoza Brazil, lakini Dunga alisisitiza kuwa ana ujuzi
wote wa kutimiza majukumu hayo.
Tabasamu! Neymar aliungana na Oscar (kushoto), David Luiz na Alex baada ya Dunga kutangaza taarifa hiyo.
Dunga aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Mandarin Oriental mjini Miami: "Tayari imeamuriwa, Neymar ndiye nahodha".
"Neymar amekubali majukumu haya vizuri
kabisa. Ni mchezaji anayependa changamoto na anapenda kushinda.
Tulizungumza naye kuhudu hilo na tulimwambia tunachokitaka.
Aliongeza: "Ni mchezaji mwenye sifa zote, licha ya umri wake ana uzoefu. Nahodha anatakiwa kuwaongoza wenzake"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni