STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 7 Septemba 2014

SIMBA SC YAFUTA MPANGO WA KUREJEA ZENJI, YAWEKA CHIMBO DAR....JUMAMOSI KUIVAA NDANDA FC NANGWANDA SIJAONA


WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, jumamosi ya wiki hii watakabiliana na timu mpya ya ligi kuu soka Tanzania bara, Ndanda FC  katika mchezo wa pasha pasha kuelekea ligi kuu ndani ya dimba la Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Simba Walioitandika Gor Mahia mabao 3-0 jana uwanja wa Taifa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki watasafiri kuelekea Mtwara ijumaa ya wiki hii tayari kwa kuwafuata wapinzani wao waliotamba kuwafunga wakali hao wa Msimbazi.
Mabao ya Simba jana yalifungwa na Mkenya, Paul Kiongera aliyetungua mawili na moja likafungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Baada ya mechi ya Mtwara, Mnyama atarejea Dar es salaam kuendelea na programu ya mazoezi kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu bara dhidi ya Coastal Union, Septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wachezaji wote wa Simba leo walipewa mapumziko na kocha mkuu Patrick Phiri na kesho wataanza mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani, jijini Dar es salaam.
Badala ya kurejea Zanzibar baada ya mechi ya Gor Mahia,  kama ilivyoelezwa awali na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, vijana wa Patrick Phiri wanaingia kambini kesho katika Hoteli ya Shynovo, maeneo ya Africana, Mbezi, Beach, Dar es salaam tayari kwa mawindo ya ligi kuu.
Kabla ya kambi inayoanza kesho, Simba ilijichimbia Zanzibar ambako ilicheza mechi tatu za kirafiki na kushinda zote.
Ilianza kwa kuichapa Kilimani City mabao 2-1, halafu ikaitandika Mafunzo 2-0 na kumalizana na KMKM kwa kutoa kipigo cha mabao 5-0, mechi zote zilipigwa Zanzibar.
Mechi ya jana ilikuwa ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki tangu kurejea kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri.
Simba ilicheza vizuri katika mechi hiyo na kukonga nyoyo za mashabiki na viongozi wa kalbu hiyo.

Wachezaji wa Simba walitandaza soka chini, wakapiga pasi za uhakika na kushambulia kwa mipango na kuibuka na ushindi mnono dhidi ya mabingwa wa Kenya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox