STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 7 Septemba 2014

RIO FERDINAND ADAI MANCHESTER UNITED ITAJUTIA KUMUUZA DANNY WELBECK ARSENAL

Bad decision: Rio Ferdinand believes Man United may live to regret the decision to sell Danny Welbeck
  Rio Ferdinand anaamini Man United   wanaweza kujuta kumuuzaDanny Welbeck

BEKI wa zamani wa Manchester United,Rio Ferdinand  amekiri kushangazwa na maamuzi ya Louis van Gaal kumuuza Danny Welbeck kwa wapinzani wao wa ligi kuu, klabu ya  Arsenal.
Welbeck aliyetokea katika akademi ya Manchester United aliuzwa Emirates siku ya mwisho ya dirisha la usajili majira ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 16 baada ya Van Gaal kuona nyota huyo wa kimataifa wa England hatakuwa na namba Old Trafford.
Mkongwe huyo alisema hata kama Welbeck alifanya vizuri, Wayne Rooney na Robin Van Persiea walimfanya asionekane kitu kwa United.
Ferdinand akiongea na gazeti la The Sun la jumapili, alizungumzia kitendo cha Welbeck kujiunga na Arsenal: "Siamini kama United wamemruhusu Welbeck kuondoka, hususani kwenda Arsenal. Kwa upande wangu naona ni kuchanganyikiwa".
"Ni mchezaji hatari kwa mabeiki na kama Arsenal watamtumia kiusahihi, atakuwa mtu hatari kwao"
"Nadhani hakuonekana sana United kwasababu hata kama alifanya vizuri, Robin van Persoe na Wayne Rooney walikuwa mbele yake. Sitashangaa kuona wanajutia kutombakisha Danny".
Mechi ijayo, Ferdinand atakutana na Man United kwa mara ya kwanza tangu alipomaliza miaka 12 kuichezea klabu hiyo na kujiunga na QPR.
Big money move: Welbeck joined rivals Arsenal after being given permission to leave Old Trafford
Usajili wa mkwanja mkubwa: Welbeck alijiunga kwa mahasimu wa United, Arsenal baada ya kupewa ruhusu ya kuondoka Old Trafford

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox