Mwenyekiti wa Yanga sc, Yusuf Manji alitangaza kuwa Emmanuel Okwi hatacheza Simba sc kwasasa ana mkataba na klabu ya Jangwani
Na
Baraka Mbolembole
Suala la mshambulizi, Mganda, Emmanuel Okwi
limekwisha. Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji imempa ruhusa ya kujiunga na
klabu yoyote mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Uganda
Wakati,
Yusuph Manji alipotoa tamko la kuitaka TFF kutoa adhabu kwa Okwi na klabu ya
Simba baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa muda mfupi na timu ya Simba.
Manji alisema Okwi bado ni mchezaji bado ni mchezaji halali wa Yanga hadi
katikati ya mwaka, 2016, huku akisisitiza kuwa klabu yoyote inayomtaka
italazimika kulipa ada ya uhamisho, dola za Kimarekani 500, 000.
Kama taarifa hiyo ingetolewa na kiongozi wa
chini labda isingekuwa na maana kwa walio wengi, lakini kutoka kwa mwenyekiti
ilichochea kitu kikubwa. Kwanza ni kuhakikisha kama kweli TFF inauwezo wa
kusimamia kanuni na sheria zake, kwa maana kama ingebainika ni kweli Simba na
Okwi walivunja sheria kila mmoja alitegemea adhabu kulingana na makosa hayo na
si ' maamuzi ya busara' kama ilivyozoeleka.
Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akiwa na Emmanuel Okwi (kulia)
Lakini sivyo, Okwi ni mchezaji
huru, hana mkataba na Yanga na alikuwa na uhuru wa kufanya mazungumzo na klabu
yoyote kwa kuwa mkataba wake wa awali na Yanga ulikuwa chini ya miezi sita.
Licha
ya Okwi kutokuwa na mkataba na timu ya Yanga, TFF imetoa taarifa kuwa mchezaji
huyo anaidai klabu ya Yanga Tsh.160 millioni! Manji alikuwa tayari kupoteza
sifa zake kama kiongozi makini?.
Achana na matukio yaliyopita chini ya uongozi
wake. Alimfuta kazi kocha, Tom Saintfiet ndani ya miezi baada ya timu kufungwa
mchezo mmoja. Wakati ule, nilisema kwa sababu alifanya hivyo kwa sababu tu
aliambiwa na Tom ' yeye ni mfanyabiashara, na si mfanyabiashara wa kimataifa'.
Tom
alikuwa mtu wa pili kumkosoa, Manji hadharani baada ya awali Iman Madega
kufanya hivyo wakati akiwa mwenyekiti wa Yanga na Manji akiwa mfadhili. Kama
binadamu mwenye mapungufu, Manji pia anaweza kufanya makosa. Lakini makosa yake
hayapaswi kufanyika mara kwa mara katika utawala ambao nyuma yake watu wengi
wanakuwa na matarajio wa kufanya kinachotakiwa.
Enzi hizo Okwi (kulia) akiwa Yanga sc
Jambo la busara kwa Manji hivi
sasa ni kuitisha mkutano na vyombo vya habari na kuomba samahani kwa upotoshaji
aliotoa kuhusu mkataba wa Yanga na Okwi. Kujiuzulu ni jambo la kiungwana, hasa
linapotokea jambo linalokugusa moja kwa moja katika utawala wa walio wengi,
kusarenda ni kitu ambacho hakihepukiki kwa Manji, vinginevyo ataendelea kuwa
kiongozi asiyeaminiwa na wale anaowaongoza kwa kuwa ni mdanganyifu, hivyo
anaweza kufanya hivyo katika jambo kubwa zaidi ya hili la Okwi.
Je, pesa inamaliza matatizo au matatizo
yanamaliza pesa? Yanga wanadaiwa na Okwi, na si Yanga kumdai Okwi. Mchezaji
huru husajiliwa bure. Baada ya kucheza mechi 13 na kufunga mabao matano, Okwi
amecheza zaidi na vifungu vya sheria na kuwazidi ujanja wanasheria wa Yanga
tangu wakati ule akitafuta jinsi ya kutoka Tunisia na kuwa huru. Millioni 100+
millioni 160 kuna namna ya wana-Yanga kumchunguza mwenyekiti wao na kupitia
upya mikitaba iliyopo. Manji amejitoa ' kafara' katika suala la Okwi,
alijivisha ' bomu' asiloweza kutegua.
Itashangaza
kuona suala la Okwi linakosa hata mtu wa kuwajibika. Upande wangu, Manji ni mtu wa kwanza
anayetakiwa kuachia nafasi yake. ' Amechafuka ', Wako wapi wanasheria wa
Yanga?. Hoi!, Okwi ameingiza pesa huku akicheza mpira katika vifungu vya
sheria. Sasa ni wakati wa wachezaji wazawa kuamka na kujiamini. Usipolipwa
miezi mitatu, wamevunja mkataba wako,…..
0714
08 43 08
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni