Big Bullets waliodaiwa kuharibikiwa na gari wakija
Tanzania kucheza na Yanga, jana jioni walitoka 0-0 dhidi ya EPAC United
katika mchezo wa ligi kuu nchini Malawi.
YANGA SC jana ilitarajia kucheza mechi ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya Big Bulltes (zamani Bata Bullets) ya Malawi
katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mechi hiyo iliandaliwa na chama cha soka cha mkoa
wa Dar es salaam, DRFA.
Jumamosi usiku baadhi ya viongozi wa Yanga na DRFA
walikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema Big Bullets wameshawasili
nchini kwa usafiri wa barabara na walikuwepo Mbeya kuelekea Dar es salaam.
Saa 5 kabla ya mechi kuanza uwanja wa Taifa, Yanga
walitangaza taafrifa za ghafla kwamba mechi hiyo haipo kwasababu Big Bullets
hawajawasili nchini.
Ilielezwa gari walilokuwa wakisafiria Big Bullets
liliharibika njiani kabla ya kuingia nchini.
Lakini kukawa na mkanganyiko, inawezekanaje timu
iripotiwe kuwepo Mbeya tena na wahusika, halafu gari liharibike nje ya mpaka wa
Tanzania. Kwa maana hiyo timu ilikuwa haijagusa mpaka wa Tanzania.
Niliwasikiliza viongozi wa DRF kwa umakini jana,
kikubwa walichoeleza ni kwamba Big Bullets walipata matatizo na walikuwa na
mawasiliano ya karibu sana mpaka usiku ‘mkubwa’ wa jumamosi.
DRFA wanasema jitihada za kutengeneza gari la timu
hiyo ziligonga mwamba na ndipo wakachukua maamuzi ya kuahirisha mechi na
jitihada za kutafuta timu nyingine ziligonga mwamba.
Pia waliwaomba radhi mashabiki kwa usumbufu
uliojitokeza. Kwa upande wa Yanga, hawakuwa tayari kuelezea kilichotokea zaidi
ya kusema DRFA waulizwe.
Walikuwa sahihi kujibu hivyo kwasababu DRFA ndio
walikuwa waandaji, lakini hawakwepi lawama ya kuwaangusha mashabiki wao
kwasababu walishindwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi taarifa za ujio wa timu
hiyo.
Kuahirishwa kwa mechi hiyo kulileta usumbufu
mkubwa kwa mashabiki hasa waliotoka nje ya Dar es salaam.
Wengine walipata taarifa wakiwa njiani kwenye
mabasi, wakati wengine hawakupata kabisa mpaka walipofika uwanjani na kukuta
hakuna dalili ya mechi.
DRFA walifanya makosa juu ya hili, ingawa sipingani
na kuwepo kwa sababu zilizo nje ya uwezo kama gari kuharibika.
Lakini mwisho wa yote, jana usiku iliripotiwa kuwa
timu ya Big Bullets jana jioni ilikuwa na mchezo wa ligi kuu nchini Malawi (TNM)
dhidi ya EPAC United, uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre.
Mchezo huo mkali na wa kusisimua ulimazika kwa
suluhu ya bila kufungana.
Kwa matokeo ya jana, Big Bullets walifikisha
pointi 36 katika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 17, sawa na vinara
Moyale Barracks ambao wanaongoza kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa.
Timu iliyokuwa na mechi ya ligi nchini Malawi, pia
ilikuwa njia kuja Tanzania, lakini iliharibikiwa na gari njiani. Ni Big Bullets
hii ninayoifahamu au kuna nyingine?
Labda walituma kikosi cha pili cha Big Bullets
kuja kucheza Tanzania, lakini mbona DRFA hawakueleza hivyo?
Matokeo ya ligi ya Malawi wikiendi (jumamosi na
jumapili) iliyopita kwa mujibu wa Mtandao wa SOCCERWAY.
Sat
|
06/09/14
|
|||||
Sun
|
07/09/14
|
|||||
3 : 0
|
||||||
2 : 1
|
||||||
3: 0
|
Kwa sasa dunia imebadilika, si rahisi tena
kudanganya kama zamani.
Wakati ambao mtu mwenye uwezo alikuwa anaweza
kuona kitu kwenye TV halafu akawaambia wasio na TV kuwa nimeota itakuwa hivi.
Kila kitu kipo wazi, Napata shida kujua kama kweli
DRFA walikuwa na mawasiliano na Big Bullets.
Kama ndio hii iliyocheza ligi kuu nchini Malawi,
basi tuna safari ndefu katika utawala wa mpira wa mpira wa miguu.
Labda DRFA watakuja kutolea ufafanuzi zaidi ya taarifa yao ya jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni