STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

ANCELOTTI AJA JUU KWA KUFANANISHWA NA MOURINHO.

MENEJA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amedai hajawahi kufananisha mafanikio yake katika klabu hiyo na ya kocha Jose Mourinho. Kocha huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain alichukua nafasi ya Mourinho mwaka 2013 baada ya kocha huyo kuisaidia timu hiyo kushinda taji la La Liga, Kombe la Mfalme na Kombe la ligi katika miaka mitatu aliyokuwepo Santiago Bernabeu. Hata hivyo, inadaiwa aliondoka katika klabu hiyo kwa utata kufuatia taarifa za kutoelewana na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na kushindwa kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ancelotti alionekana kufikia mafanikio hayo katika msimu wake wa kwanza kwa kuwafunga mahasimu wao Atletico Madrid katika mchezo wa fainali huku
pia
akishinda Kombe la Mfalme na Kombe la Ligi. Matokeo hayo yanafanya wawili hao kulinganishwa mafanikio yao katika timu hiyo lakini Ancelotti amejitoa katika ulinganyisho huo na kudai kuwa yeye anajaribu kufanya kazi yake kila siku katika ubora. Ancelotti amesema hajawahi kulinganisha mafanikio yake na Mourinho katika klabu hiyo kwnai ana mambo mengi ya kufikiria huku akijaribu kuisaidia timu hiyo iweze kufanya vyema zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox