MCHEZAJI mkongwe wa
zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amesema mshambuliaji nyota wa timu
hiyo Mario Balotelli anapaswa kuachwa na badala yake achukuliwe Raheem
Sterling kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real
Madrid. Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan amekuwa na msimu mgumu
toka asajiliwe kwa kitita cha euro milioni 20 na kukosa nafasi katika
mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Queens Park Rangers. Kutokana na
umuhimu wa mchezo wao huo wa kesho utakaochezwa Anfield, Garragher
anadhani kuwa meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers hapaswi kuhatarisha
kwa kumpanga Balotelli kwasasa yuko katika kiwango cha chini. Carragher
amesema Balotelli hazunguki vya kutosha uwanjani hivyo katika mchezo na
timu kama Madrid unahitaji aina ya wachezaji wenye nguvu na wanaocheza
kwa juhudi na sio kutembea uwanjani.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumanne, 21 Oktoba 2014
BALOTELLI HAPASWI KUCHEZESHWA MECHI YA MADRID - CARRAGHER.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni