STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 21 Oktoba 2014

RAIS WA ZAMANI WA SANTOS ADAI MADRID WALITOA DAU KUBWA KULIKO BARCELONA KATIKA USAJILI WA NEYMAR.

RAIS wa zamani wa klabu ya Santos, Luis Alvaro de Oliviera Ribeiro amedai kuwa Real Madrid walitoa dau kubwa zaidi kuliko Barcelona mwaka uliopita lakini Neymar mwenyewe aliamua kwenda Camp Nou. Mshambuliaji huyo alisajiliwa na Barcelona kwa kitita cha euro milioni 86.2 katika majira ya kiangazi mwaka jana na kumaliza msuguano wa miaka kadhaa kati ya timu hizo katika kugombea saini ya Neymar. Ribeiro amesema wakati akipokea matibabu alimuachia majukumu makamu wake ambaye alikuja kuchukua kiti hicho baadae Odilio Rodrigues kuendelea kufanya mawasiliano na Barcelona na Madrid. Rais huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa Rodrigues alimfuata na kumhabalisha kuwa Madri wametoa ofa kubwa lakini tatizo ni kwamba mchezaji mwenyewe anataka kwenda Barcelona. Kutokana na hilo Ribeiro amesema walikuwa hawana ujanja zaidi ya kufuata matakwa ya mchezaji mwenyewe na kumuuza kule anapopahitaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox