STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 21 Oktoba 2014

DI MARIA ATAKUWA FITI KUIVAA CHELSEA - UNITED.

KLABU ya Manchester United ina uhakika kuwa Angel Di Maria atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Chelsea pamoja na kupata majeruhi katika mchezo wa jana dhidi ya West Ham United. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alikwua akisikia maumivu katika kifundo cha mguu na kutolewa nje katika dakika ya 76 ya mchezo huo huku akionekana kuwekea barafu katika eneo hilo wakati akiwa benchi. Hata hivyo imedaiwa kuwa Di Maria amefanyiwa vipimo katika uwanja wa mazoezi wa United leo kwa ajili ya tahadhari lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid anatarajiwa kuwa fiti katika mchezo dhidi ya Chelsea. Di Maria mwenye umri wa miaka 26 amekuwa katika kiwango bora toka atue Old Trafford ambapo tayari ameshatengeneza nafasi nne katika mechi sita huku akitengeneza nafasi ya bao alilofunga Marouane Fellaini katika mchezo wa jana uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox