STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 7 Oktoba 2014

CASILLAS AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSIANA NA BIFU LAKE NA MOURINHO

Kipa Iker Casillas amesema aliamua kukaa kimya, kutojibizana na aliyekuwa kocha wake, Jose Mourinho sababu ya kulinda maslahi ya Real Madrid.

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi Iñaki Gabilondo katika mahojiano maalum, Casillas alisema haikuwa sahihi kuzozana na Mourinho huku akijua inayoathirika zaidi ni Madrid.
“Ningeweza kumjibu Mourinho, nilinyamaza kwa manufaa ya klabu. Sikuona kama ni sahihi kuwasha moto ambao ungeuunguza klabu.
“Hatukuwa tukizungumza vizuri hata kwenye mikutano ya waandishi tulienda wote, lakini hatukuzungumza.
“Mwanzo sikujua kama walikuwa na matatizo na mimi, lakini nilipoumia ndiyo nikagundua kuna kitu.
“Kwani hata baada ya kurudi kutoka majeruhi, kila siku msaidizi wake aliendelea kusema sikuwa fiti na mashindano.
“Taratibu nilianza kugundua kuna kitu kati yetu, mwisho nikagundua ni tatizo,” anafafanua Casillas.
Kipa huyo aliingia katika hali ya kutoelewana na Mourinho wakati akiwa kocha wa Madrid na alikuwa kocha wa kwanza kuanza kumtupa benchi nahodha huyo wa Hispania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox