Mlinda lango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Iker Casillas
ndiye bado anashikilia rekodi ya kuwa mlinda lango anayelipwa pesa
nyingi duniani kwa kazi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa
na jarida la The Richest la mwaka 2014.
Casillas anakula kitita cha pauni milioni 6.30 kwa mwaka sawa na bilioni
1.26 pesa za kitanzania kwa mwaka. Casillas ni mmoja wa walinda lango
wanoheshimiwa sana nchini Hispania na ndiyo maana ni nahodha wa klabu
yake ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, pengine ni kwa sababu
ni zao la football academy za nchini humo.
Iker Casillas alikuwa mlinda lango wa timu ya taifa ya Hispania wakati
timu hiyo inachukuwa ubingwa wa mataifa ya Ulaya mwaka 20008 baada ya
kushindwa kufanya hivyo kwa takriban miaka 44 iliyopita. Mbali na
mafanikio hayo, goli kipa huyo pia alisaidia Hispania kuchukuwa kombe la
dunia mwaka 2010.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni