Mlinda lango nyota na mwenye heshima kubwa Stanford Bridge, Petre Cech
amefunguka kwenye vyomba vya habari leo hii na kusema kama ataendelea
mlinda lango chaguo la pili (namba 2) katika klabu ya Chelsea, ni baro
akaondoka na kutafuta klabu nyingine itakayompa nafasi ya kwanza.
Cech alipata jera kubwa katika bega lake la kushoto msimu uliopita
wakati Chelsea ikipepetana na Atletical Madrid mwezi July katika
mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya hali iliyomfanya yeye kumalizia
msimu wa 2013/2014 akiwa nje ya dimba tangu pale alipo pata majeraha na
nafasi yake kuchukuliwa na Mark Schwarzer kabla ya Thibault Courtois
kurejea Chelsea akitokea Atletical Madrid alipokuwa akicheza kwa mkopo.
Cech akitolewa nje baada ya kuumia bega la kushoto wakati Chelsea
ikabiliana na Atleticala Madrid dimbani Vicente Calderon msimu uliopita
katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mchezo ambao ulikwisha kwa
timu kutoka suluhu.
|
Petre Cech ni mmoja wa wachezaji nguli katika klabu ya The Blues, kwani
mpaka sasa amedumu klabu hapo kwa takaribani miaka 10, huku akifanikiwa
kuichezea klabu hiyo michezo 500. Lakini, tangu msimu wa 2014/2015 uanze
Cech hakuendelea kuwa golikipa chaguo namba moja katika klabu ya
Chelsea kwani mlinda lango anayechipukia kwa kasi,Thibault Courtois 22,
ameoneka kufanya vizuri sana kitendo kilichomfanya Jose Mourinho
kumuamini zaidi.
Huyu pia ni goli kipa bora wa ligi kuu nchiniUingereza msimu uliopita wa 2013/2014
|
Cech amekariri akilalama kuwa, haoni sababu yeye kusugua benji akiwa
kama chaguo namba mbili kwa Mourinho kwani kuna michezo mikubwa na
migumu ipo mbele yake kama vile, michuano ya mabingwa wa Ulaya ya 2016
pamoja na majukumu makubwa aliyonayo katika timu ya taifa, hivyo kucheza
kama chaguo namba mbili kwa Chelsea anaona ni hatari sana kwani
anaamini itadhoofisha uwezo wake.
Petre Cech alichechea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu msimu huu uanze
wakati Chelsea ikicheza dhidi ya Arsenal Juma pili iliyopita Dimbani
Stanford Bridge, baada ya Courtois kuumia. Mchezo huo ulimalizika kwa
Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, kichapo ambacho kiliendelea
kumpa Arsena rekodi mbaya ya kuchezea kichapo mara kwamara wanapokutana
na Chelsea kwa muda mrefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni