STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

MADEREVA WA LANGALANGA WATAKA MAELEZO KUFUATIA AJALI YA BIANCHI.

DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga kutoka timu ya Force India, Sergio Perez amedai kuwa ajali iliyomuacha dereva Jules Bianchi na majeraha ya kichwa, haikubali na iliweza kuepukika. Perez ambaye ni raia wa Mexico amesema madereva lazima watalitaka shirikisho la mashindano hayo-FIA kutaka ufafanuzi wa kile kilichotokea na hatua zitachukuliwa kuepuka hali hiyo. Perez aliendelea kudai kuwa wanapaswa kupewa majibu ya kina wa kitu gani haswa kilitokea katika ajali hiyo mbaya. Bianchi kwasasa anaendelea vyema ingawa bado yuko katika chumba cha uangalizi maalumu baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kuligonga trekta lililokuwa pembezoni wakati mashindano ya Japan Grand Prix Jumapili iliyopita. Perez amesema inatakiwa hatua mpya za makusudi zichukuliwe ili kuwepo na gari la usalama popote ambapo trekta linatumika kwa ajili ya kuondoa magari yaliyopata hitilafu lkatika mashindano hayo ili kuepuka kujirudia kwa ajali kama hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox