STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

NILIHATARISHA SOKA LANGU KWA AJILI YA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA - RONALDO.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebainisha kuwa aliweka soka lake hatarini kwa kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid msimu uliopita pamoja na kusumbuliwa na majeruhi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alikutwa na tatizo hilo mwishoni mwa msimu wa 2013-2014 lakini halikumzuia kutocheza mchezo huo walioshinda mabao 4-1 dhidi ya Atletico huku yeye akifunga bao moja. Hata hivyo Ronaldo sasa amekiri kuwa ilikuwa bora zaidi kwa mwili wake kupumzika badala ya kucheza mchezo huo. Ronaldo amesema ni kweli alijiweka katika hatari kwa kucheza fainali hiyo iliyochezwa jijini Lisbon lakini katika maisha huwezi kushinda kitu kama muda mwingine hutaweza kujiweka katika hatari. Nyota huyo aliendelea hakuna mchezaji anayependa kukosa fainali ya Ligi ya Mabingwa au michuano ya Kombe la Dunia ndio maana alijisukuma hivyohivyo na kuamua kucheza. Hata hivyo Ronaldo amesema jitihada zake zililipa kwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa huku akifunga bao lakini mambo hayakwenda akiwa na timu ya taifa ya Ureno kwani walienguliwa mapema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox