STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 8 Oktoba 2014

OZIL "PANCHA" TENA, KUKAA NJE WIKI TATU.

KIUNGO wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil amekwenda jijini Munich leo kufanyiwa vipimo vya goti lake la kushoto na kuacha wasiwasi juu ya nafasi yake ya kuwemo katika kikosi cha nchi hiyo kitakachovaana na Poland jijini Warsaw katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016. Ozil ambae alicheza dakika zote 90 katika mchezo Arsenal waliofungwa mabao 2-0 na Chelsea Jumapili iliyopita anaweza kuwa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa katika kikosi cha Joachim Loew kukosekana baada ya Bastian Shweinsteiger na Marco Reus kutokuwepo. Msemaji wa timu hiyo ya Ujerumani Jens Grittner amesema Ozil amekuwa na matatizo ya goti lake la kushoto lakini hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapopata vipimo. Hata hivyo kuna habari nzuri kwa Loew baada ya Julian Draxler kukiunga na kikosi cha timu hiyo leo baada ya kupona mafua yaliyokuwa yakimsumbua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox