VILABU vikubwa barani
Ulaya vinatarajia kulitaka Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kucheza
michuano ya Kombe la Duniani mwaka 2022 nchini Qatar katika kipindi cha
mwezi Mei. Qatar ilishinda haki za kuandaa michuano hiyo mwaka 2010
lakini mjadala wa kuhamisha michuano hiyo kutoka katika majira ya
kiangazi kama ilivyozoeleka umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwaka. Chama
cha Vilabu Ulaya-ECA ambacho kinajumuisha klabu za Manchester United,
Liverpool, Barcelona na Bayern Munich vimejadili kuwa kipindi cha mwezi
Mei mwaka 2022 kitakuwa muafaka kwa michuano hiyo. ECA wanaamini
michuano hiyo kuchezwa katika kipindi cha majira ya machipuko kitasaidia
kupunguza hatari iliyopo ya kucheza katika joto kali. Maswali yaliibuka
haraka baada ya Qatar kupata haki ya kuandaa michuano hiyo kuhusu
uwezekano wake kutokana na joto kali lililopo katika nchi hiyo ya jangwa
katika kipindi June na Julai ambacho ndio Kombe la Dunia huchezwa. Ila
mara zote Qatar wenyewe wamekuwa wakisisitiza wanaweza kuandaa michuano
hiyo kiangazi kwa kutumia mpango wao wa vipoza hewa ili kupunguza joto
nmdani ya viwanja na sehemu ambazo zitakuwa zimetengwa kwa ajili ya
mashabiki.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 24 Oktoba 2014
VILABU ULAYA VYAITAKA FIFA KUKUBALI KOMBE LA DUNIA 2022 KUCHEZWA MEI.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni