STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 4 Desemba 2014

BAADA YA KUTUA SIMBA.... SSERUNKUMA -“GOR MAHIA ITABAKI KUWA MOYONI MWANGU”


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mchezaji bora wa dunia mara mbili Mreno Cristian Ronaldo amekuwa akiimwagia sifa Manchester United mara kwa mara licha ya kwamba yeye kwa sasa ni mali ya Klabu ya Real Madrid ya Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Jambo hilo pia limejitokeza kwa mshambuliaji Mganda Dan Sserunkuma ambaye leo amemwaga wino wa kuitumikia klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
se
Sserunkuma imethibitishwa rasmi na uongozi wa Simba SC kwamba atakuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba watakaoikabili Yanga SC katika mechi ijayo ya ‘Nani Mtani Jembe 2′ dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 13 baada kusaini mktaba wa miaka miwili wa kuwatumikia wanamsimbazi.
Sserunkuma, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) alitua jijini jana usiku na kusaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva baada ya mkataba wake na Gorl Mahia ya KPL kumalizika.
Mara tu baada ya kusaini mkataba huo utakaomuweka Msimbazi hadi Desemba 3, 2016, Sserunkuma ameimwagia sifa mabingwa wa Kenya, Klabu ya Gor Mahia kwa kumlea vizuri katika miaka miwili na nusu aliyoitumikia.
Amesema Gor Mahia itazidi kubaki moyoni mwake huku akiwamiminia sifa mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuunga mkono katika kipindi chote alichokuwa na klabu hiyo pamoja na wakala wake, Ken Joseph na familia yake.
“Nilifurajia maisha ya miaka miwili na nusu Gor Mahia, lakini huu ni wakati sahihi wa kusema kwa heri. Tulikuwa na nyakati nyingi za kufurahi na za mafanikio ya pamoja, na mashabiki walikuwa wakiniunga mkono sana – hasa tulipokuwa katika wakati mgumu.
“Gor Mahia itabaki kuwa moyoni mwangu na ninamshukuru kila mtu ndani ya menejimenti ya klabvu hiyo kwa kunipa nafasi nyingi za mafanikio kuonesha kipaji changu.
“Pia ninaishukuru familia yangu na wakala wangu kwa sapoti yao kubwa kwangu. Sasa ninaangalia mbele kufungua ukurasa mwingine wa maisha yangu – nikiichezea Simba,” amesema Sserunkuma.
Akiwa Gor Mahia, Sserunkuma alitwaa taji la Ligi ya Timu Nane nchini Kenya (Top 8 Cup), Ngao ya Hisani na ubingwa wa KPL mara mbili mfululizo huku akiibuka mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu (2014).
se 1
Sserunkuma atakuwa na faida ya kucheza pamoja na Mganda mwenzake Okwi katika safu ya ushambuliaji ya Simba baada ya kuondolewa kwa Kiongera ambaye anakwenda India kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia baada ya kugongana na kipa Shaban Kado wa Coastal Union katika mechi yao ya kwanza ya sare ya bao moja msimu huu wa VPL kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 21.
Sserunkuma aliyezaliwa Desemba 14, 1989 (umri wa miaka 24 ambao hata hivyo, una utata kwa wanaofuatilia kwa kina soka la Afrika Mashariki) jijini Kampala, Uganda amekuwa katika kiwango cha juu tangu ajiunge na Gor Mahia 2012 akitokea Nairobi City Stars.
Simba wanaamini mkali huyo wa kufumania nyavu atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chao ambacho kimeonekana kuwa butu msimu huu kikiwa kimefunga mabao nane tu katika mechi saba za VPL, idadi ambayo ni sawa na mabao yote ya Tambwe katika mechi saba (akicheza sita) za mwanzo wa msimu uliopita wa ligi hiyo.
Mbali na Kiongera na Sserunkuma, Simba ina nyota wengine wanne wa kigeni ambao ni Waganda Emmanuel kwi na Joseph Owino pamoja na Warundi Amissi Tambwe na Pierre Kwizera.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox