STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 4 Desemba 2014

MOURINHO KUMPA KIBARUA DROGBA AKISTAAFU SOKA.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema mshambuliaji wake Didier Drogba bado atakuwa na kazi Stamford Bridge wakati akiamua kustaafu rasmi kucheza soka. Drogba mwenye umri wa miaka 36 kwasasa anaichezea kwa mara ya pili klabu hiyo huku akifunga bao katika mchezo wa jana ambao Chelsea waliibugiza Tottenham Hotspurs kwa mabao 3-0. Akihojiwa Mourinho amesema jambo ni kwamba nyota huyo atamalizia soka lake akiwa na Chelsea na inavyoonekana anaweza kubakia akifanya mambo mengine pindi atakapostaafu. Drogba amefanikiwa kushinda mataji 10 akiwa na Chelsea mara ya kwanza kati ya mwaka 2004 mpaka 2012 huku akifunga mabao 157 katika mechi 341 alizocheza. Nyota huyo alijiunga tena na Chelsea katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kuondoka klabu ya Galatasaray ya Uturuki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox