STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Desemba 2014

PIGO: CHELSEA KUMKOSA COURTOIS KESHO.

KLABU ya Chelsea imepata pigo baada ya golikipa wake Thibaut Courtois kupata majeruhi ya msuli kuelekea katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Hul City. Golikipa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anaungana na Cesc Fabregas anayetumikia adhabu kuwa wachezaji ambao wataukosa mchezo huo wakati Chelsea wakijaribu kurejesha makali yao baada ya kipigo kutoka kwa Newcastle United mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na wanahabari meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema Courtois alikuwa na matatizo madogo wakati wa mazoezi hivyo hatakuwepo katika mchezo wa kesho. Mourinho aliendelea kudai kuwa Fabregas amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake lakini hawatakuwa naye katika mchezo wa kesho akitumikia adhabu yake ila wana wachezaji wengine anaowaamini. Mourinho sasa atalazimika kuendelea kumtumia Petr Cech ambaye alimtumia pia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon Jumatano iliyopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox