STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Desemba 2014

WENGER AZIDI KUWAKERA MASHABIKI WA ARSENAL KWA KUDAI HANA MPANGO WA KUSAJILI JANUARI.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amehatarisha kuwaudhi zaidi mashabiki wa timu hiyo baada ya kudai kuwa hatakuwa na haja ya kufanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwakani kama wachezaji wote katika kikosi chake cha sasa watakuwa fiti. Kocha huyo raia wa Ufaransa amekuwa katika shinikizo kubwa katika wiki za karibuni baada ya Arsenal kuonekana kushindwa mapema mbio za ubingwa kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City. Wenger alishambuliwa na mashabiki wenye hasira katika kituo cha treni wakati akirejea London baada ya mchezo dhidi ya Stoke. Pamoja na kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13 Wenger bado bado anaonesha kutoshtushwa na hali hiyo kwa kudai kuwa hatarajii usajili wa Januari kuwa pilikapilika kubwa. Wenger amesema kama wachezaji watakuwa fiti na uwezo wa kucheza hadhani kama atahitaji kufanya usajili wa aina yeyote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox