STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 10 Januari 2015

MAN U MKWANJA MREFU KUMNG'OA BALE REAL MADRID

Manchester United imeripotiwa imepiga hatua nyingine katika mbio zake za kumnyakua winga Gareth Bale baada ya Real Madrid kuonekana kukubali ofa yao kwa mchezaji huyo.
United wanaiwania kwa udi na uvumba saini ya Bale baada ya msimu kumalizika, kikosi hicho cha Louis van Gaal kikihitaji mchezaji mwenye kiwango cha juu.
Imeripotiwa kuwa kiasi cha pauni milioni 150 kimeandaliwa kwa ajili usajili huo, huku ripoti zaidi zikieleza jana kuwa Madrid sasa wameonekana kukubali ofa hiyo.
Madrid watafanya biashara hiyo kama ofa hiyo itawafikia na wameripoti kuwa tayari wameshaanza kusaka mbadala wake, wakimtaka mchezaji wa Borussia Dortmund, Marco Reus.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox