Kiungo
mshambuliaji wa Chelsea Oscar yupo katika rada za mabingwa wa Italia
Juventus, ambao wanaamini ni mbadala sahihi wa Andrea Pirlo ambaye
anaelekea ukingoni( Daily Mail).
Chelsea
wamefungua mazungumzo na wakala wa Radamel Falcao ili kuangalia
uwezekano wa kuipata saini ya Mkolombia huyo katika msimu huu wa usajili
wa majira ya joto (Gianluca di Marzio).
Wawakilishi
wa Liverpool wamekutana na Piero Ausilio kuangalia uwezekano wa kuipata
saini ya Mateo Kovacic. Mkolombia huyo mwenye umri wa miaka 21 ana
thamanii ya Euro milioni 30 ambayo ni sawa na Paundi milioni 21
(Calciomercato.com).
Inter
Milan wako mbioni kutuma ofa ya Euro milioni 36 kumnasa Mkolombia Juan
Cuadrado na kumrejesha Italy baada ya msimu m'baya akiwa na klabu ya
Chelsea tangu aliposajiliwa kutokea Fiorentina (Daily Mirror).
Liverpool
wameambiwa na Southampton wanatakiwa kuongeza kiasi cha Paundi milioni
10 na kufikia 15 ili kumsajili beki namba 2 wa klabu hiyo Nathaniel
Clyne katika kipindi hiki cha usajili kinachokaribia (Daily Mirror).
Manchester
United watupilia mbali mpango wao wa kutaka kumsajili beki wa kulia wa
Southampton Nathaniel Clyne na kuwaachia nafasi Liverpool kuendelea na
mbio hizo (PA Sport).
Idrissa
Gueye, kiungo raia wa Senegal, anaweza kujiunga na Southampton ndani ya
siku chache zijazo, huku mazungumzo yao yakifikia mahali pazuri.
Southampton wanajiandaa kutekeleza hilo endapo kiungo wao raia wa
Ufaransa Moragan Schneiderlin ataondoka. Ada ya uhamisho ya Gueye
inakadiriwa kuwa ni Euro milioni 10 (L'Equipe).
Dayot
Upamecano, 16, atajiunga na Manchester United akitokea katika klabu ya
Valenciennes. Kinda huyo akiwa na timu ya Ufaransa chini ya umri wa
miaka 17 alishinda michuano ya mataifa ya Ulaya. Pia anaweza kuigharaimu
Man United kiasi cha Euro 450,000 (L'Equipe)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni