STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 28 Juni 2015

BRAZIL 'OUT' COPA AMERICA, YACHAPWA NA PARAGUAY


Brazil imetupwa nje ya michuano ya michuano ya Copa America kwa mikwaju ya penati kufuatia kwenda sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Paraguay kwenye dakika 90 za mchezo na kuufanya mchezo huo kuamuriwa kwa matuta ndipo Brazil walipotupwa nje ya mashindano kwa penati 4-3 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye dimba la Ester Roa Rebolledo huko Chile.
Brazil ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika za kawaida (90’) kupitia kwa Robinho aliyeifungia timu yake dakika ya 15 kipindi cha kwanza akiunganisha krosi maridadi aliyogongewa na beki wa pembeni wa FC Barcelona Dani Alves na kuipa timu yake matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya mataifa huko bara la America ya Kusini.
Robinho vs ParaguayLakini dakika ya 70 matumaini hayo yaliota mbawa baada ya Derlis Gonzalez kuisawazishia Paraguay kufuatia Thiago Silva kuunawa mpira kwa makusudi katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo kuamua ipigwe penati kuelekea kwenye lango la Brazil. Gonzalez hakufanya ajizi, akaukwammisha mpira kambani kwa penati ambayo ilimuacha Jefferson golikipa wa Brazil akikosa la kufanya kuuzuia mpira huo.
GonzalezKipindi cha pili kilikuwa na upinzani mkali kutokana na Paraguay kutawala mchezo kwa muda mwingi na kupata nafasi kadhaa za kufunga lakini uimara wa golikipa wa Brazil Jefferson uliisaidia Brazil kuhimili mikikimikiki ya Paraguay.
Paraguay vs Brazil 1Kutupwa nje ya michuano hiyo kwa Brazil limekuwa ni pigo jingine kwao baada ya lile la awali la kufungiwa kwa nyota wao na nahodha wa timu hiyo Neymar, Neymar alifungiwa kucheza mechi nne na kupigwa faini ya dola 10,000 za kimarekani baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kumpiga na mpira Pablo Armero wakati Brazil ikicheza dhidi ya Colombia kwenye mchezo wa kundi C.
Paraguay vs BrazilMatokeo hayo yanaifanya Paraguay kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na Argentina ambayo ilifuzu jana usiku kwenye mchezo wake wa kukata na shoka dhidi ya Colombia ambao pia uliamuliwa kwa mikwaju ya penati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox