STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 28 Juni 2015

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA ARSENAL KUHUSU ARTURO VIDAL


Wakati huu mashabiki wa Arsenal wakisubiri golikipa wa Chelsea, Petr Cech kujiunga Emirates, kuna taarifa mpya kwamba kiungo wa Chile na Juventus, Arturo Vidal naye yuko mbioni kutua Kaskazini mwa London.

Vidal ambaye anaitumikia Chile katika michuano ya Copa America inayoendelea katika ardhi yao,  kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kutua England hususani katika klabu ya Manchester United.

Leo tetesi zimeibuka kwamba Vidal ataondoka Juventus majira haya ya kiangazi na tayari amekubali dili la kujiunga na Arsenal ambalo litatangazwa baada ya Copa America kufikia tamati.
Tetesi hizo zimeibuka saa chache zilizopita kutoka kwa Mwandishi wa habari wa Chile, Hernan Feler ambayo amethibitisha kwenye radio kwamba Arsenal wamemsajili Vidal.
Feler ni chanzo makini cha habari? bado haijulikani, lakini idadi kubwa ya mashabiki wa Arsenal wanadai ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza taarifa za Alexis Sanchez kutua Arsenal kutokea Barcelona.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox