STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 24 Juni 2015

CAVANI MGUU NDANI MGUU NJE COPA AMERICA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez ameonyesha matumaini yake kuwa Edinson Cavani atabakia katika kikosi chake baada ya baba wa mshambuliaji huyo kukamatwa kufuatia kupata ajali ya barabarani. 

Nyota huyo wa Paris Saint-Germain ameripotiwa kutojua la kufanya kama abakie au arudi nyumbani Uruguay kuwa na baba yake kufuatia ajali hiyo aliyopata juzi. 

Hata hivyo, Cavani alionekana akifanya mazoezi na wenzake jana wakati wakijiandaa na mchezo wao robo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya wenyeji Chile baadae leo. 

Tabarez aliwaambia wanahabari kuwa Cavani atapewa muda wa kuamua mwenyewe kuhusiana na suala hilo. 

Vyombo vya habari nchini Uruguay vimeripoti kuwa kijana mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akiendesha pikipiki alifariki kwa kugongwa na gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na baba yake Cavani. 

Mzee huyo alikamatwa baada ya ajali hiyo huku uchunguzi ukiendelea kujua chanzo chake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox