KIUNGO ABASRIM CHIEDEBERE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUWASILI MJINI TANGA AMBAKO AMEJIUNGA COASTAL UNION AMBAYO AMESAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA. |
Coastal Union leo imefanikiwa kumsajiili straika wa wa Stand United Abasalim Chidiebele kwa mkataba wa mwaka mmoja, straika huyo atakitumikia kikosi cha ‘Wagosi wa Kaya’ kwa msimu ujao wa 2015-2016
Chidiebele alimaliza ligi akiwa ndiye mfungaji bora wa klabu ya Stand United ‘Chama la wana’ iliyopanda daraja kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye msimu uliomalizika akitupia kambani jumla ya mabao 11 na kusaidia klabu hiyo ya mjini Shinyanga isiporomoke daraja.
Mnaijeria huyo amejiunga na kikosi hicho cha jijini Tanga ikiwa ni mpango wa kikosi hicho kujiimarisha kwa ajili ya mchakamchaka wa ligi kuu ya msimu ujao kutokana kutofanya vizuri kwenye michezo ya ligi kwa msimu uliopita.
Kikosi cha Coastal Union kilikuwa ni miongoni mwa timu ambazo zilipambana kukwepa kushuka daraja ambapo bado kina kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi yake kwenye uwanja wa Taifa kwa kipigo kikali cha goli 8-0 kutoka kwa Yanga na kuweka rekodi ya kuwa timu iliyofungwa magoli mengi kwa msimu uliopita. Kutokana na hali hiyo, kikosi cha Wagosi wa Kaya kimeanza kujiimarisha mapema ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao ambao utaanza mwezi Agosti mwaka huu.
Mbali na Coastal Union, Kagera Sugar na Mbeya City zilionesha nia ya kutaka kumsajili mkali huyo ambaye alikuwa ni tegemeo kwenye safu ya wafumania nyavu ya Stand Unidet kwa muda wote alioichezaea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni