STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 17 Desemba 2015

RONALDO KUJENGA HOTEL MIJI MBALIMBALI DUNIANI..............

 Ronaldo has announced four hotels, to open in four different cities - Funchal, Lisbon, Madrid and New York

Cristiano Ronaldo tayari ameanza kujipanga na maisha baada ya soka baada ya kukiri kwamba siku zake za kuendelea kuwa mmoja wa wacheza soka zipo mbioni kumalizika miaka kadhaa ijayo.
  Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 anategemewa kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu na ana mipango tayari kwa ajili ya maisha yake ya baadae – leo alhamishi amezindua mpango wake wa kujenga hotel zake kubwa za kifahari za ‘CR7 Hotels’ katika miji ambayo ina uhusiano na maisha yake ya soka: Funchal, Lisbon and Madrid – na nyingine katika
mji wa New York – mahala ambapo kunatajwa ataenda kumalizia soka lake.


Cristiano Ronaldo akiwa na Dionisio Pestana, mmiliki wa Pestana Hotel Group, jijini Lisbon leo

Nahodha huyo wa Ureno ameingia kwenye makubaliano na kushirikiana na kampuni ya  Pestana Hotel Group katika ujenzi wa hotel zake hizo. Ronaldo anasema haya ni maandalizi ya maisha yake baada ya soka.

‘Kazi yangi ni kucheza soka, lakini maisha hayawezi kuwa kila siku hivi. Nimeamua kuanzisha hii project na itafanikiwa kwa sababu nina timu ya watu wazuri wanaonizinguka. 
‘Mimi bado kijana lakini nafikiria maisha yangu ya mbele, ya mwanangu na familia yangu. 

Hotel ya kwanza inategemewa kufunguliwa kipindi cha kiangazi mnamo mwaka 2016, jijini Madeira, ambapo Ronaldo alizaliwa. Itafuatiwa na Hotel jijini Lisbon – mahala ambapo aliitumikia klabu yake ya Sporting Lisbon – mwishoni mwa mwaka 2016. Hotel ya jijini Madrid inatarajiwa kuzinduliwa mwaka 2017.

Ronaldo alitania: ‘Mimi nitakuwa nashughulikia vitanda!’ 
Aliongeza:Nafahamu uwekezaji huu ni salama na naweza kuutegemea katika siku za mbeleni.’

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United bado hajaweka wazi mahala amabpo atajenga hotel nchini England, ingawa hotel ya jijini New York itafunguliwa 2017. 

 
Hotel ya kwanza itafunguliwa Madeira, nina furaha sana kwa hili, ya pili itakuwa Madrid, mahala ambapo nijacheza. Hii ni biashara kubwa zaidi katika maisha yangu na ninajisikia amani sana kuifanya. 

‘Mwanzoni tulikuwa tunafikiria kufungua hotel moja tu, hivyo kuanza na hotel 4 kwa mpigo ni mwanzo mzuri sana. Ni kama umeanza kucheza soka na ukafunga magoli mengi. 

Wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes alikuwepo wakati wa uzinduzi wa project hiyo ya Ronaldo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox