STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Juni 2015

HII HAPA ADHABU YA JARA BAADA YA KUMDHALILISHA CAVANI.

BEKI wa timu ya taifa ya Chile, Gonzalo Jara anatarajiwa kukosa michezo inayoendelea ya Copa America baada ya kunyukwa adhabu ya kutocheza mechi tatu kwa kosa la kumshika makalio mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani. 

Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-Conmebol limedai kuwa wamefikia uamuzi kutokana na beki huyo kuonyesha tabia isiyokuwa ya kiuanamichezo. Mbali na adhabu hiyo lakini Jara ametundikwa faini ya dola 7,500. 

Tukio hilo lilitokea wakati Chile waliposhinda bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika Alhamisi iliyopita. 

Cavani alimtundika kibao Jara baada ya kufanyiwa kitendo hicho hatua ambayo ilipelekea mwamuzi kumlima kadi ya pili njano na hivyo kutolewa nje. 

Adhabu hiyo inamaanisha Jara ataukosa mchezo wa leo wa nusu fainali dhidi ya Peru pamoja na mechi nyingine ya aidha fainali au kutafuta mshindi wa tatu kutegemeana na matokeo watakayopata leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox